Baadhi ya watanzania wamekuwa wanazisahau tamaduni zao na kuiga tamaduni za kigeni,hali hii imekuwa ikisababisha matatizo kwa kizazi cha sasa kwani wengi wamekuwa wakizisahau tamaduni zao na kujikita kwenye tamaduni za kigeni.Nchi nyingi za afrika wanavazi la taifa lao hata Tanzania pia inalo lakini hawalidumishi vile ipasavyo,kwani wamekuwa wakivaa mavazi ya kigeni hata kwenye maadhimisho ya sherehe za kitamaduni.Hali hii imekuwa ikiwaumiza baadhi ya watu wanao hitaji kulijua vazi la taifa lakini wamekuwa wakishindwa kutambua ni lipi kwani utandawazi unaadhiri tamaduni zetu watanzania.

|
vazi la khanga limevaliwa toka miaka ya zamani sana.lakini zamani vazi hili lilikuwa halina mauwa na rangi,lilikuwa jeupe kama sanda.
|

|
Nchi ya Tanzania ina makabira mengi lakini kwa asilimia kubwa kabila la wamasai wamekuwa wakidumisha mila zao kuanzia miaka ya zamani mpaka sasa.
|